Thursday, September 5, 2013

Mikononi mwa polisi ya Sugu yajirudia Bungeni

Tazama picha tatu za Mheshimiwa Sugu akitolewa bungeni........akiwa mikononi mwa polisi kama alivyoimba

askari wa bunge na wabunge wengine wakimzuia a wengine wakitaka atoke
                         

akishikilia mic
akiburuzwa atoke nje

Chanzo cha vurugu zile ni "Ukosefu wa Busara Ndogo Tuu toka kwa Naibu Spika!"
Hadhi ya KUB(kiongozi wa kambi ya upinzani) ni sawa kabisa na Waziri Mkuu, kitendo cha Naibu Spika kumzuia KUB asizungumze, kumuamuru akae chini na kisha kuamuru atolewe nje, "that was provocation kwa wapinzani wote wa kweli!", kiliwatia hasira, na kilichofuata ni actions in provocation!. Chanzo ni ukosefu wa busara ndogo tuu wa Naibu Spika!.

Laiti Mhe. Naibu Spika, angelimruhusu KUB kuzungumza na kuisikiliza hoja yake!, naamini 100% kwa 100%, yote yaliyofuatia yasingetokea!.

Bungu letu lina mapungufu makubwa na ya msingi ya kikanuni za uendeshaji mabunge ya vyama vingi!. Kiukweli kila kunapotokea vurugu bungeni, mimi huwa namkumbuka sana Mhe. Samuel Sitta!.

Kiukweli huko nyuma nimewahi kulalamikia sana uendeshaji wa bunge wa Madam Spika, Mhe. Anna Makinda, lakini sasa sasa nakiri, pamoja na mapungufu yake yote ya kibinaadamu, Mhe. Anna Makinda is better of 100 times than Mhe. Job Ndugai!. This man is a disaster!.

No comments:

Post a Comment